Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imewataka wananchi wanaoishi karibu na Migodi mikubwa ya Madini ya (Buzwagi na Bulyankulu ) kufanya kazi zingine mbadala za kuwaingizia vipato badala ya kutegemea ajira katika migodi hiyo ili kuondokana na migogoro isiyokuwa na tija baina yao na wawekezaji.
Kauli hiyo imetolewa na jana na Mkuu wa wilaya ya Kahama ANAMRINGI MACHA katika Hafla maalum ya kumtambulisha Mzabuni aliyeshinda Dhabuni ya kuzoa Taka ngumu hususani vyuma chakavu katika mgodi wa Bulyankulu, AZAN LOGISTIC CO.LTD ya Kahama.
Amesema kuwa baada ya kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji wa madini katika migodi hiyo baadhi ya wananchi wanao ishi karibu Migodi hiyo wamekuwa tegemezi kwa kutojihusisha na kazi zingine za uzalishaji mali na kuwataka wafanye kazi za ujasiriamali.
Katika Hatua nyingine MACHA ameitaka Kampuni ya AZAN LOGISTIC kutoa ajira kwa Wazawa pindi atakapoa anza kutoa huduma hiyo katika mgodi huo ili kuwapa hamasa wananchi kupenda kufanya kazi na wawekezaji wazawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, AZAN SAID SALUM ameahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wa Mji mdogo wa Kakola ambapo Mgodi huo upo na kuahidi kuwa kampuni yake itaajiri walimu wawili wa sayansi katika shule mbili za sekondari katika Halmashauri ya Mslala.
Mbali na hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, SAIMON BEREGE ametolea ufafanuzi suala la upimaji wa viwanja kwa kusema kuwa tayari Kampuni za upimaji zinaendelea na upimaji ili kuhakikisha wananchi wanarasimishiwa makazi yao ambapo kwa awali viwanja elfu 10 vitapimwa.
Kampuni ya AZAN LOGISTICS imeshida dhabuni hiyo ambapo kwa sasa itatoa huduma ya kuzoa vyuma chakavu katika mgodi wa Bulyankulu kwa Muda wa Mwaka mmoja na miezi 10.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment