Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Yapendekeza TANESCO Igawanywe

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imependekeza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kugawanywa na kuwa mashirika mawili ili kuepuka hasara.

Hayo yameelezwa  jana Jumanne Mei 28, 2019 na msemaji wa kambi hiyo wa Wizara ya Nishati, John Mnyika wakati akiwasilisha  maoni ya wapinzani bungeni.

Alisema kwa kipindi kirefu Tanesco inajiendesha kwa hasara, akitolea mfano kwamba  tangu utawala wa  Serikali ya Awamu ya Nne ilikuwa ikipata hasara ya Sh124 bilioni.

Alibainisha kuwa  takwimu zinaonyesha baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani, shirika hilo linapata hasara kubwa zaidi, kwamba  hadi  2017 ilipata hasara ya Sh346 bilioni sawa na ongezeko la Sh122 bilioni.


from MPEKUZI

Comments