Jumla ya Miradi 88 ya Maji hapa nchini imejengwa chini ya Kiwango kwa kipindi cha mwaka 2010 na 2015 hali iliyosababisha pawe na kero kubwa ya uhaba wa maji hususan Maeneo ya vijijini hadi sasa.
Hayo yamesemwa Mei 29,2019 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa wakati akijibu swali mbunge Wa Moshi Vijijini Anthony Komu aliyehoji serikali inafanya mpango gani wa kubainisha waliohusika na mapungufu yaliyobainika na kuwachukulia hatua.
Katika majibu yake Prof.Mbarawa amesema kuna miradi 88 ya Maji Tanzania imejengwa chini ya kiwango kwa mwaka 2010 hadi 2015 na nia ya serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha watanzania wanapata Maji ya Uhakika na kama mradi umejengwa chini ya Kiwango serikali bado inafanya uchunguzi na ikishakamilisha hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya waliohusika.
Katika hatua nyingine Prof.Mbarawa amesema serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwa kushirikiana na mkandarasi wa barabara wameweza kukarabati na kumaliza tatizo la uvujaji maji barabarani kwa gharama ya Tsh. Mil.1 laki 4 na 37 elfu[1,437,000/=]
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment