Waziri Ummy Azitaka Halmashauri Kote Nchini Kuhakikisha Zinatenga Bajeti Maalum Kwa Ajili Ya Kutekeleza Mikakati Ya Kupambana Na Malaria
Ikiwa leo ni Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo huadhimishwa April 25 ya kila mwaka , Waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha kuwa wanatenga bajeti maalumu kwa ajili ya kutekeleza mikakati mbalimbali ya kupamba na malaria.
Waziri Ummy ametoa rai hiyo April 24 ,jijini Dodoma alipotembelea katika kituo cha afya cha Makole Mkoani Dodoma kwa ajili ya kukabidhi vyandarua vyenye dawa viuatilifu katika kutekeleza adhma ya serikali ya kuwakinga akina mama wajawazito pamoja watoto dhidi ya ugonjwa wa malaria.
Aidha, waziri ummy amesema kuwa kati magonjwa ambayo yanaongoza kuua watanzania ni ugonjwa wa malaria lakini habari njema ni kwamba toka serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aingie madarakani wameweza kutekeleza mikakati mbalimbali ya kutokomeza malaria nchini Tanzania.
Mbali na hilo amesema kuwa akina mama wajawazito wanatakiwa kuhudhuria kliniki mara tu wanapo gundua kuwa ni wajawazito huku akibainisha mikakati mbalimbali wanayo itekeleza kama serikali kupitia wizara ya afya kwaajili ya kutokomeza malaria .
Kwa upande wake Fransis Bujiku ambaye pia Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa lakini pia anaratibu kitendo cha udhibiti wa Malaria mkoa wa Dodoma , amesema kuwa kwa mwaka 2015 kulikuwa na kiwango cha maambukizi kwa asilimia moja na kwa kiwango hicho wameweza kukishusha mpaka asilimia 0.6 hivyo ni mafaniko makubwa.
Akizungumza kwa niaba ya akina mama waliopokea msaada huo , mmoja wa akina mama hao, Amina Alphonce ameishukuru wizara ya afya kwa kuwapatia vyandarua hivyo kwani vitawasaidia katika kujikinga na ugonjwa wa malaria pamoja na kutoa ushauri kwa wakina mama wenzake kuwa na tabia ya kuhudhuria vituo vya afya.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Malaria mwaka huu 2019 ni ‘’ Zero Malaria inaanza na Mimi’’.
from MPEKUZI

Comments
Post a Comment