Urusi imesema wanajeshi wake wataendelea kubakia Venezuela kwa muda wote watakaohitajika kubakia na kuyapinga madai ya rais wa Marekani Donald Trump ya kuitaka iondoe wanajeshi wake katika nchi hiyo inayokabiliwa na mgogoro.
Hatua ya Urusi ya kupeleka wanajeshi pamoja na vifaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa nia ya kumuimarisha rais Nicolas Maduro imezusha wasiwasi mkubwa kimataifa kuhusu mgogoro wa Venezuela ambako utawala wa rais Trump unatia msukumo wa kufanyika mabadiliko ya kiutawala.
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesisitiza leo kwamba wanajeshi wake waliko Venezuela hawasababishi kitisho cha aina yoyote kwa mtu yoyote.Maria Zakharova msemaji wa wizara hiyo amesema jeshi la Urusi nchini Venezuela linahusika katika utekelezaji wa makubaliano ya shughuli za kijeshi na ushirikiano wa kiufundi na wataendelea kuwepo huko kwa kipindi watakachohitajika kuwepo..
Credit:DW
Credit:DW
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment