Katika kukabiliana na changamoto ya Usafiri kwa maofisa elimu mikoa,Serikali kupitia TAMISEMI imenunua takribani magari 26 kwa ajili ya Maofisa elimu mikoa katika mikoa yote 26 Tanzania bara .
Hayo yamesemwa Machi 27 jioni , jijini Dodoma na Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo wakati akifunga mkutano mkuu wa 6 wa maafisa elimu wilaya na mikoa Tanzania bara[REDEOA] ambapo amesema kuwa magari hayo yatarahisisha usafiri kwa maafisa hao katika kutembelea shule mbalimbali katika mikoa yao na kuibua changamoto na kuzifanyia ufumbuzi.
Mhe.Jafo amesema huwa hapendi suala la uzembe katika ufuatiliaji hivyo amemwagiza katibu mkuu wizara ya TAMISEMI ndani ya siku tisini magari hayo yawe yameshapatikana na kukabidhiwa kwa maafisa elimu wa mikoa.
Waziri Jafo amewataka Maafisa Elimu,Kujituma ,kujitoa na kuzipenda kazi zao huku akiwataka kuwaheshimu na kuwahurumia watu wa chini yao wakiwamo walimu na kuacha dhana ya kuwadharau na badala yake kuwatia moyo ili wafundishe kwa kujituma.
Aidha ,Waziri Jafo amebainisha kuwa wizara yake hadi kufikia sasa imeshatenga fedha zaidi ya Tsh.Bil.18 kwa ajili ya vifaa vya maabara kwa shule 1200 hapa nchini.
Katika hatua nyingine Waziri huyo wa TAMISEMI amezungumzia juu ya suala la nidhamu ambapo amebainisha katika kizazi hiki kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakivaa mlegezo wakiwa wanafundisha .
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Elimu wilaya na mikoa Tanzania bara , [REDEOA] Bi.Germana Mung’aho ambaye ni afisa elimu kutoka mkoani Mtwara amesema mambo yote waliyojadili watayachanganua huku akiwashukuru wajumbe wote kwa kushiriki mkutano huo muhimu.
Mkutano mkuu wa Maafisa elimu wilaya na mikoa Tanzania
bara[REDEOA]Umekutanisha maafisa elimu mikoa na wilaya kutoka mikoa yote 26 Tanzania bara na kaulimbiu ya mwaka huu ilikuwa ni Elimu bora itatufikisha katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment