Rais Magufuli Asimulia Alivyogoma Kuongea na Waziri Mwakyembe Baada Ya Taifa Stars Kufungwa Na Lesotho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amefichua siri ya kutozungumza na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe mara baada ya Taifa Stars kupoteza mchezo wake dhidi ya Lesotho Novemba 2019.

Rais Magufuli amefunga hayo wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Kamati ya Uhamasishaji ya timu ya Taifa pamoja na Bondia Hassani Mwakinyo ikiwa ni siku moja baada ya timu ya taifa kufuzu michuano ya Mataifa Afrika.

"Tangu tulipofungwa na Lesotho na huku Mil. 50 zangu zikiwa zimeliwa iliniuma kweli kweli, sikuwahi kuongea na Mwakyembe tangu siku ile hadi leo nilipompigia, aliniandikia meseji kuwa tuwe na Kombe la Magufuli, kama ilivyo Kagame Cup, sikumjibu.

“Kabla ya mchezo ule nilizungumza naye akiwa Afrika Kusini akaniambia timu iko safi na mchezo huu lazima tushinde na matokeo yake wakafungwa.”

“Nilikuwa nikiangalia ile mechi naona kuna mapungufu, iliniuma kweli, kwa sababu inaniumiza kweli kwa nchi kama Tanzania yenye watu milioni 55 mnakwenda kufungwa na nchi yenye watu milioni 2,” amesema

 
Mamilioni ya watanzania jana walikuwa na furaha kufuatia timu ya taifa ya Tanzania kuichapa Uganda kwa mabao 3 kwa sifuri na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa manne yaliyofuzu fainali za AFCON zitakazofanyika Juni 2019, nchini Misri.


from MPEKUZI

Comments