Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Na Diwan Mmoja Watangaza Kuhamia CCM Wakitokea CUF

Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Diwani wa kata ya Tandika, Geoffrey Isack Mwachisye pamoja na Diwani wa Kata ya Chikongola Musa Namtema (Fasheni) leo 27 March 2019, wametangaza rasmi kujiunga na chama cha Mapinduzi(CCM) wakitokea Chama cha wananchi (CUF).

Wawili hao, wamesema sababu kubwa ya wao kujiunga CCM,  ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa,John Pombe Magufuli.


from MPEKUZI

Comments