Mkurugenzi wa Mipango TAKUKURU Kulthum Mansoor, ambaye Machi 28, 2019, alitajwa na Rais Magufuli kwa tuhuma za kuwadhulumu viwanja, baadhi ya wafanyakazi wenzake wa TAKUKURU amekamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi Oysterbay.
Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, Kulthum alikamatwa jana Alhamisi Machi 28, 2019 na kupelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay, jijini Dar es Salaam ambapo leo Ijumaa March 29 atafikishwa mahakamani
Jana, Rais Magufuli akizungumza Ikulu mara baada ya kumuapisha Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mlowola pamoja na kupokea ripoti ya Takukuru alisema anashangazwa kwa taasisi hiyo kutomchukulia hatua.

from MPEKUZI
Comments
Post a Comment