Jiji La Dodoma Kwa Kushirikiana Na Sumatra Latangaza Barabara Mpya 9 Za Mabasi [routes ]zinazounganisha Mji Wa Serikali Pamoja Nauli Zake .

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin ametangaza utaratibu mpya uliowekwa na halmashauri yake katika mzunguko wa magari ya abiria yaani daladala ambao utaanza kutumika siku za karibuni.

Akizungumza jana  Machi 20  na waandishi wa habari ,Kunambi  amezitaja barabara hizo kuwa ni pamoja na barabara ya Kutoka mnada mpya kwenda mji wa serikali kupitia sabasaba umbali wa km 42.5 nauli ni Tsh.700,Veyula kwenda mji wa serikali kupitia sabasaba  umbali wa km 42 nauli Tsh.750. 

Barabara zingine ni barabara  ya  St.Gemma  kwenda mji wa serikali kupitia Sabasaba  km 39 nauli Tsh.700,barabara ya Swaswa  kwenda mji wa serikali kupitia sabasaba  umbali wa km 32  nauli Tsh.600,barabara ya Mkonze  kwenda mji wa serikali kupitia sabasaba umbali wa km 35 nauli Tsh.650,barabara ya  Benjamin Mkapa kwenda mji wa Serikali  kupitia sabasaba umbali wa km  29 nauli Tsh.600. 

Barabara zingine ni Udom/Utumishi  kwenda mji wa serikali kupitia Sabasaba  km  35  nauli Tsh.650,barabara ya Udom/Utumishi  kwenda mji wa serikali  kupitia Iyumbu  km 16  nauli Tsh.450,na mzunguko wa ndani wa mji wa serikali nauli ni Tsh.400. 

Hata hivyo Kunambi amezungumzia jitihada ambazo jiji linafanya kuhakikisha linajenga miundombinu rafiki katika mji wa Serikali kwa kushirikiana na TARURA.


 


from MPEKUZI

Comments