Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Katibu wa timu ya Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [Bunge sports],Mhe.William Ngeleja amewahakikishia Watanzania kuwa Bunge litakuwa pamoja na Watanzania katika kuitakia ushindi mnono timu ya Taifa Stars dhidi ya Uganda hapo Jumapili Machi 24 katika kujiweka vyema katika mashindano ya AFCON 2020.

Mhe.Ngeleja ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Sengerema mkoani Mwanza ameyasema hayo leo Machi 22 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa kitengo cha habari bungeni jijini Dodoma.
Ngeleja amesema kuwa Bunge lina imani kubwa na timu ya taifa Stars pamoja na benchi la ufundi lililoteuliwa na waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe.
Amesema kila mtanzania kwa imani yake anatakiwa kuiombea timu ya Taifa Stars kushinda katika Mchezo huo ili iweze kusonga mbele zaidi.
Naye kocha mkuu wa timu ya Bunge[Bunge Sports] Mhe.Venance Mwamoto ambaye ni mbunge wa Kilolo Mkoani Iringa amewaasa watanzania kuwa na uzalendo na timu yao kwa kuvaa jezi za Taifa la Tanzania wakati wakishangilia popote pale .
Aidha Mhe.Mwamoto amewaasa watanzania kushangilia Mwanzo mwisho ili kuipa hamasa ya Kushinda timu hiyo.
Hata hivyo Mhe.Ngeleja na Mhe.Mwamoto wameiahidi Timu ya Taifa Stars kuwa Bunge lipo tayari kuwasaport pindi wafanyapo vizuri la litaishauri serikali kuongeza bajeti kwenye timu ya Taifa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment