Waziri wa Kilimo: Asilimia 60 ya wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu nchini sio wazalishaji

Asilimia 60 ya wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu wanakuwa sio wazalishaji  kutokana na kusubiri ajira mbalimbali katika Serikali, Mashirika na taasisi mbalimbali  huku wakiacha kilimo ambacho ndiyo chenye ajira kubwa na ya moja kwa moja huku wakiacha  Kilimo Biashara ambacho ndiyo suluhisho la ajira kwa vijana nchini.

Hayo ameyasema Waziri wa Kilimo Mh.  Japhet Hasunga wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na Kongamano la vijana  Kimataifa kuhusu Kilimo Biashara (Youth Agro Summit International) litakalofanyika Machi 20 hadi 22 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Serikali imesema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda tunahitajika kuwekeza nguvu kwa vijana kuingia katika Sekta ya Kilimo na kuacha kuzunguka na bahasha ya kaki ya kuomba ajira sehemu mbalimbali katika mashirika na taasisi nchini.


“Vijana wakiingia katika Kilimo suala la kutembea na bahasha kwa ajili ya kutafuta ajira  litakuwa historia kwani kijana kuendesha Kilimo  hakuhitaji watu wa kufanya usaili”amesema Hasunga.

Hasunga amesema kuwa serikali imedhamiria kuweka mazingira ya Kilimo kwenda kisasa kwa kuhakikisha masoko ndani yanakuwa nafasi na ziada kuuza nje ya nchi.

Aidha amesema Kilimo kimekuewa kikilimwa kwa mazoea na kufanya kilimo kuonekana kigumu lakini serikali ya awamu ya tano tunakwenda na Kilimo cha kisasa kwa kuhusianisha masoko pamoja na viwanda kwa kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao.

Hasunga amesema nchi yeyote duniani inategemea vijana katika kupata Maendeleo  hivyo serikali haitawaacha nyuma vijana katika sekta ya Kilimo na biashara.

Amewataka  vijana  kuwa na mwamko wa elimu huku wengine wakiwa wataalam katika fani mbalimbali jambo ambalo  litawatafanya kuwa chachu ya Kilimo na biashara  na kufanya vijana  waliokata tamaa kuingia katika sekta hiyo.

Amesema takwimu zinaonyesha asilimia 53 ndio wanatumia jembe la mkono katika kilimo huku asilimia 27 wakitumia wanyama katika kuendesha katika kuendesha kilimo chao wakati  takwimu zinaonyesha  asilimia 20 wanatumia trekta .

Nae Mwenyekiti wa Kongamano la Vijana Kimataifa Kuhusu Kilimo Biashara Majabi Emmanuel amesema kuwa  wanatarajia kuwa na washiriki 1000  kutoka sehemu mbambali wa ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa wameandaa Kongamano hilo kutokana na vijana kujitenga katika kilimo wakati ndio chenye fursa ya kujiajiri moja kwa moja.


from MPEKUZI

Comments