Kesi ya viongozi wa CHADEMA kuendelea leo

Kesi inayowakabili baadhi ya Viongozi Wakuu wa Chama cha CHADEMA itaendelea leo, Alhamis, Januari 31, 2019, kwa kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

viongozi hao ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16 mwaka jana Dar es Salaam.


from MPEKUZI

Comments