Hukumu ya ‘Malkia wa Tembo’ Kutolewa Februati 15

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imepanga kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo kukutwa na meno ya tembo inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan maarufu kama ‘malkia wa meno ya Tembo’ Februari 15, mwaka huu.

Mbali na mshtakiwa huyo,washtakiwa wengine ni, Salvius Matembo na Phillemon Manase.

Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, aliyesikiliza kesi hiyo baada ya pande zote mbili Jamhuri na utetezi kuwasilisha majumuisho ya mwisho.

Januari 28, mwaka huu mahakama hiyo ilipokea majumuisho ya mwisho kwamba washtakiwa wana hatia au la.

Hakimu alisema mahakama yake itatoa hukumu Februari 15, mwaka huu. Awali upande wa Jamhuri uliita mashahidi 11 na utetezi watatu.

Upande wa Jamhuri katika kesi hiyo uliongozwa na Mawakili wa Serikali Wakuu, Faraja Nchini, Paul Kadushi na Wakili wa Serikali, Salim Msemo.

Msemo alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kusikilizwa hukumu.

"Mahakama yangu itasoma hukumu dhidi ya washtakiwa Februari 15, mwaka huu" alisema Hakimu Shaidi.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh.bilioni 13, kinyume cha sheria.


from MPEKUZI

Comments