Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake sita leo Jumanne Januari 29, 2019 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Maimu na wenzake hao jana Jumatatu Januari 28, 2019 walifutiwa mashtaka na mahakama hiyo lakini muda mfupi baadaye washtakiwa hao walikamatwa tena na polisi.
Wamefikishwa mahakamani hapo leo asubuhi na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu kilichopo mahakama hapo.
Hata hivyo, haijajulikana watapandishwa mahakamani saa ngapi na kujibu mashtaka gani.
from MPEKUZI

Comments
Post a Comment