TSNP Yawaangukiwa TAKUKURU Rushwa ya Ngono Vyuoni

Mtandao  wa   Wanafunzi   Tanzania    (TSNP)    imeitaka    Taasisi    ya    Kuzuia    na    Kupambana    na    Rushwa (Takukuru) kuongeza jitihada  zaidi  za  kuwajengea  uwezo 
wanafunzi     na     wahadhiri     juu     ya   masuala   ya   rushwa   hasa   ya   ngono kwa lengo la kupunguza au kumaliza kabisa tatizo hilo vyuoni.

TSNP  umesema  kuwa  rushwa  ya   ngono   kwa   sasa   imeshamiri   katika   vyuo   mbalimbali   nchini   hivyo  inapaswa  kukemea  kwani  inaharibu   maisha   ya   wanafunzi   ambao      wanategemewa      kuwa      viongozi wa baadae.

Akizungumza    na    waandishi    wa   habari   jijini   Dar   es   Salaam   hivi   karibuni,   Katibu   wa   TSNP,   Joseph  Marekela  alisema  rushwa  ya  ngono  vyuoni  ni  changamoto  kubwa  hasa  kwa  wanafunzi  wa  kike  hivyo  jitihada  za  makusudi  zinahitajika  ili  kuhakikisha  kuwa 
hakuna    mtu    anayepoteza    haki    yake ya msingi kwa kukataa kutoa rushwa   hiyo   ambayo   si   tu   inapoteza utu wa mtu bali ni kinyume na haki za binadamu.

Alisema   mfumo   wa   upimaji   uwezo    uliyopo    sasa    umempa    mamlaka  makubwa  mhadhiri  ya  kuamua   hatma   ya   mwanafunzi   kitaaluma    jambo    ambalo    lina
sababisha  uwepo  wa  mianya  ya  rushwa  ya  ngono  kwa    wahadhiri  wasio  na  maadili  ambao  wanatumia  nafasi  yao  kuminya  haki  ya  mwanafunzi.

“Kwakuwa      tatizo      hili      ni      kubwa   na   limeathiri   wanafunzi   wengi  chuoni    tunatoa  wito  kwa  Takukuru waongoze jitihada zaidi kwa  kuwajengea  uwezo  taasisi  za 
Takukuru  vyuoni  ili  kupambana  na  tatizo  hili  kikamilifu,  pia  vituo  vya jinsia na Serikali za wanafunzi ziwajibike ipasavyo ili kuhakikisha kuwa   hakuna   anaepoteza   haki   yake ya msingi kwa kukataa kutoa rushwa hiyo ya ngono,” alisema.

Hata     hivyo     mtandao     huo     umesema  kuwa  ukosefu  wa  taulo  za   kujisitiri   wanafunzi   wa   kike   hasa  wa  vijijini  kipindi  cha  hedhi  inaathiri maendeleo ya wanafunzi
hao kitaaluma.

Kutokana      na      hali      hiyo,      Marekela   alisema   wanatoa   wito   kwa  Serikali  kupitiaWizara  yenye  dhamana  kulitazama  upya  suala  kwa  kugawa  bure  taulo  hizo  kwa 
wanafunzi  wa  kike  hasa  waliopo  maeneo   ya   vijijini   ili   kunusuru   ndoto zao walizojiwekea.

Aidha alisema suala la mikopo kwa  wanafunzi  wa  elimu  ya  juu  bado ni changamoto kwani wengi wao  wameshindwa  kuendelea  na  masomo kwa kukosa mikopo hiyo


from MPEKUZI

Comments