Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limeomba radhi wateja wake wa mikoa iliyounganishwa na gridi ya Taifa kwa katizo la umeme lililotokea leo Desemba 29, 2018 majira ya Saa 9:00 Alfajiri.
Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter, TANESCO imesema kwamba sababu iliyopelekea kukatika kwa umeme ni hitilafu iliyotokea katika mfumo wa gridi.
Hata hivyo taarifa hiyo imesema kwamba wataalamu na mafundi wa shirika hilo wanaendelea na jitihada za kuhakikisha umeme unarejea kwa haraka katika maeneo yote.
"Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza. Tutaendelea kutoa taarifa kadri kazi inavyoendelea. Tunawataarifu wateja wetu kuwa huduma ya umeme imeanza kurejea kwenye baadhi ya maeneo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa na Morogoro", imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment