Mbunge Mwingine CHADEMA Amtaka Waziri Mhagama Ajiuzulu Sakata la Kikokotoo

Baada ya Rais John Pombe Magufuli kufanya utenguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya mifuko ya Jamii, (SSRA)  Dr. Irene Isaka, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amedai kwamba atashangazwa kama Waziri ataendelea kuwepo ofisini.

Heche ameyasema hayo ikiwa ni siku moja kupita tangu Rais alipotangaza kuendelea kutumika kwa sheria ya zamani katika uchukuaji wa mafao.

Kupitia mtandao wa Twitter Heche amesema kwamba "Kanuni inatungwa na waziri, kwa maana nyingine kanuni ni ya waziri. SSRA ni 'regulatory body' nitashangaa 'regulator' kutumbuliwa alafu Waziri kuendelea kubaki ofisini"

Mbali na Heche kupitia mitandao ya kijamii baadhi ya Wabunge wa upinzani wamekuwa wakimyooshea kidole Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu  Jenista Mhagama kujiuzulu nafasi yake kutokana na kushindwa kutetea maslahi ya wananchi.

Jana akifuta kutumika kwa kanuni mpya Rais Magufuli alisema “Kwanza kustaafu ni heshima na siyo mateso. Mtu amefanya kazi kwa muda mrefu hata zaidi ya miaka 30 na matokeo yake unampa masharti kuwa atapata mafao kidogo. Utampangiaje mtu kuwa sasa utachukua kiasi fulani halafu kingine tutakutunzia, huu ni wema gani?” Hii haiingii akilini hata kidogo kwa mtu yeyote,”.


from MPEKUZI

Comments