Juliana Shonza Atoa Mashart TBC

Na Anitha Jonas – WHUSM – Tarakea,Rombo
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameutaka uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kuhakikisha wanaboresha usikivu wa matangazo kwa Wilaya ya Rombo katika maeneo ambayo hayana usikivu kabla ya bunge la bajeti.

Mheshimiwa Shonza ameyasema hayo jana katika kijiji cha Tarakea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro alipotembelea mitambo ya TBC iliyopo katika eneo la mpakani mwa Tanzania na Kenya kwa lengo la kutaka kufahamu kwanini  usikivu wa matangazo ya TBC bado unachangamoto japo kuwa wamefunga mitambo hiyo eneo la karibu na mpakani.

“Kero ya usikivu katika eneo hili la mpakani ni lazima lifanyiwe kazi kwa haraka kwani kikubwa hapa ilikuhakikisha mnamaliza kero hii ni mkafunge minara yenu katika eneo lenye mlima mrefu ili mawimbi yenu yaweze kwenda mbali bila kukutana na kizuizi na ili muweze kufanikiwa katika utafiti wenu wa eneo bora ni vyema muwashirikisheni wazawa wa eneo hilo katika kuwashauri eneo zuri lililopo juu zaidi,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo ameusisitiza uongozi wa Kanda ya Kaskazini TBC kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuboresha usikivu huo kwani pesa kwa ajili ya maboresho hayo ilikwisha toka na sivyema pesa hiyo ikatumika vibaya kwa kusimika mitambo hiyo katika maeneo ambayo hayatatatua kero hiyo ikaja kuwalazimu kuhamisha tena mitambo hiyo, kwani kwa kufanya hivyo hayo yatakuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma hivyo ni vyema kuliangalia hilo.

Kwa upande wa Meneja wa TBC Kanda ya Kaskazini Bw.Gerald Uisso alieleza  kuwa ofisi yake ilikuwa imekwisha fanya utafiti katika eneo la Mlima Hakwe ila kabla ya kusimika mitambo hiyo watafanya utafiti na kwa maeneo mengine kwa kuzingatia maelekezo.

“Mchakato wa kusimika mitambo katika eneo hilo ilikuwa ni baada ya kumaliza ujenzi wa kusimika mitambo katika eneo la Longido ambao unaendelea kwa sasa,”alisema Bw.Uisso.

Pamoja na Hayo nae Mkuu wa Wilaya ya Tarakea Bibi.Agness Hokororo alimweleza Naibu Waziri huyo kuwepo kwa changamoto kubwa ya wakazi wa eneo hilo kupata habari sahihi naza uhakika kwani Radio wanazosikiliza wakazi waeneo hilo niza kutoka nchi ya jirani na hiyo imekuwa changamoto kubwa kwao katika kupata taarifa za mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za serikali.

Halikadhalika Mheshimiwa Shonza aliwasisitiza uongozi wa TBC kukumbuka kuwa Shirika hilo nila umma hivyo linawajibu wa kuhakikisha linafikisha matangazo yake kila mahali  pasipo kuwa na changamoto yoyote.


from MPEKUZI

Comments