Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 38

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
“Ehee niambie”
“Mama yako amepatika”
“Kweli?”
Niliuliza kwa shauku iliyo ambatana na furaha kubwa sana.
“Ndio amepatika, ila…….”
Mwanasheria alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge kidogo.
“Ila nini?”                   
Nilimuuliza mwanasheria huku furaha yangu ambayo nilikuwa nayo ikaanza kunipotea taratibu.
“Hali yake sio nzuri, katika harakati za kumkomboa kwa bahati mbaya alipunyuliwa na risasi ya kichwani mwake na kumfanya apoteze fahamu, na ninavyo zungumza hivi sasa, wapo njiana wanakuja naye nchini humu”
Nikajikuta nikinyon’gonyea na taratibu nikakaa chini na kumfanya Camila na watu wengine kunishangaa, kwa maana ni muda mchache tu wametoka kuniona nikiwa nimejawa na furaha sana

ENDELEA
Camila akachuchumaa kwa haraka, akaichukua simu yangu mkononi mwangu na kuiweka sikioni.
“Ni Camila ni nini kinacho endelea?”
Camila aliuliza kwa shahuku kubwa sana, huku akinitazama usoni mwangu. Habari aliyo ipata hata yeye mwenyewe akaonekana kumnyong’onyeza. Muongozaji wa tangazo hili akatufwata sehemu tulipo.
 
“Vipi jamani kuna tatizo?”
Camila akaibi kwa kutingisha kichwa huku akimtazama muongozaji huyu wa filamu.
“Nahitaji kwenda uwanja wa ndege sasa hivi”
Nilizungumza huku nikimtazama Camila usoni mwake.
“Hakuna tatizo Ethan”
Muongozaji wa tangazo hili alizungumza, taratibu Camila akaninyanyua akisaidia na muongozaji huyu wa tangazo, nikaingizwa ndani ya gari, kisha baada ya muda kidogo Camila naye akaingia ndani ya gari na safari ya kuondoka eneo hili ikaanza huku tukiwa tumetanguliwa na gari la walinzi wa mama Camila. Furaha na amani vikanipote kabisa moyoni mwangu. Akilini mwangu, akili yangu inamuwaza tu mama yangu ambaye hali yake ni mbaya sana.
 
“Mume wangu usijali kila jambo litakwenda vizuri sawa?”
Nikajibu kwa kutingisha kichwa tu na safari ikaendelea. Ikatugarimu kama lisaa moja kufika katika kiwanja cha ndege. Nikamkuta mwanasheria akiwa katika eneo hili akimsubiri mama yangu kufikishwa hapa.
“Itagarimu masaa ngapi kufika hapa?”
“Kama masaa lisaa moja na dakika aroboini na tano hivi. Na nimesha andaa magadaktari bingwa. Akipokelewa ataingizwa kwenye helicopter ya hospitali na atawahishwa hospitalini”
“Nashukuru kwa kila jambo”
Nilizungumza kwa sauti ya unyonge sana. Masaa yakazidi kusonga mbele huku kila baada ya nusu saa mwana
sheria aliwasiliana na vijana tulio wapa kazi ya kwenda kumkomboa mama yangu.
“Wapo wapi?”
 
“Kama baada ya dakika kumi ndege ikatua hapa”
Mwanasheria alizungumza huku akitazama saa yake ya mkononi. Madaktari wapatao wanne wakakaa tayari kwa ajili ya kumpokea mama. Ndani ya dakika kumi alizo niambia mwana sheria, ndege maalumu ya kukodi taratibu ikatua kwenye uwanja huu. Wahudumu wa maalumu wa uwanja huu, wakaanza kukimbilia kwenye eneo ndege hiyo ilipo simama huku wakiwa wameongozana na madaktari wote wanne walio beba kitanda maalimu cha kukunjua. Sikuona haja ya mimi kuendelea kuhushudia mambo kwa mbali, nikaanza kukimbia kuelekea kule walipo. Nikafika na kukuta wakimtoa mama yangu ndani ya ndege hii, macho yakanitoka sana, kwani ni miaka mingi sana sijawahi kumuona mwana mama huyu. Kumbu kumbu kadhaa zikaanza kujirejea kichwani mwangu juu ya maisha yangu na huyu mwana mama, ila kila nilipo jaribu kuzikumbuka vizuri, nikashindwa kabisa.
“Kitanda hichi kikaanza kusukumwa hadi kwenye gari la wagonjwa, likafungwa kwa haraka na kuelekea katika uwanja mdogo wa helicopter.
 
“Mkuu kina helicopter ya kampuni, ipo hapa unaja wa ndege tayari kwa kuelekea hospitalini”
Mwanasheria alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Sawa twende”
Tukaanza kukimbia kuelekea kwenye helicopter hiyo, huku Camila naye akiwa hayupo mbali nami. Tukaingia ndani ya helicopter hiyo na safari ya kuelekea hospiyalini ikaanza. Sikuzungumza kitu chochote hadi tukafika katika uwanja wa helicopter wa hospitali hii kubwa na nzuri. Tukashuka na kupokelewa na nesi mmoja na moja kwa moja tukaanza kupelekwa kwenye chumba cha upasuaji. Uzuri wa eneo hili la chumba cha upasuaji kuna kioo kikubwa ambacho mtu ukiwa nje ya chumba hichi unaweza kuona kinacho endelea ndani ya chumba. Tukawashuhudia madaktari jinsi wanavyo endelea na kuifanya kazi yao ya kuhakikisha kwamba wanayaokoa maisha ya mama yangu yanakuwa salama. 

Baada ya nusu saa mama Camia naye akafika katika eneo hili, kwa haraka akanikumbatia kwa nguvu huku akinipiga piga mgongoni mwangu taratibu. Machozi yakanimwagika na nikashindwa kujibu kitu chochote. Dada Mery naye akafika katika eneo hili, alipo tuona kidogo akaonekana kujawa na mshangao kwa maana toka nianzishe mchakato wa kumtafuta mama yangu, sikuwahi siku hata moja kumueleza dada Mery wala bibi Jane Klopp.
“Ethan ni kitu gani kinacho endelea?”
Dada Mery alizungumza huku akinisogelea karibu yangu. Akanitazama usoni mwangu kwa sura iliyo jaa wasiwasi mwingi.
 
“Ni mama”
“Mama yupi Ethan?”
“Mama yangu mzazi”
“Ohoo jamani?”
Dada Mery alizungumza kwa upole na unyonge mkubwa sana. Taratibu akanikumbatia huku akinibembeleza, Gafla tukawaona madaktari wakiwa katika harakati harakati nyingi ndani ya chumba hicho na wakanifanya niweze kukimbilia kwenye kioo hichi na kutazama ndani. Madaktari wengine wazee wakaingia ndani ya chumba hichi jambo lililo tufanya tujawe na wasiwasi mwingi sana.
Kitu kilicho zidi kutuchanganya ni mara baada ya mapazia ya kijani kufungwa kwenye vioo hivi na tukashindwa kuona kinacho endele ndani ya chumba hichi.
 
“Ni nini kinacho endelea?”
Niliuliza kwa sauti ya unyonge, hapakuwa na mtu aliye weza kunijibu. Camila akajikaza na kunikumbatia kwa nguvu.
“Nahitaji kuingia ndani humu”
“Ethan huwezi kufanya hivyo, kumbuka madaktari wapo kwenye kazi mume wangu”
“Nimesema ninataka kuingia”
Nilizungumza kw ukali sana huku nikimuachia Camila, kila mtu anaye nitazama akaonekana kunishangaa sana kwani maamuzi niliyo yafanya ni ya ukali sana. Nikafungua malango wa chumba hichi, manesi  wawili wakaniwahi kwa haraka hata kabla sijapiga hatua yoyote.
“Tafadhali, tunakuomba uweze kutoka humu ndani Mr Ethan”
“Nahitaji kuzungumza na mama yangu”
Nilizungumza kwa sauti ya unyonge ila iliyo jaa msisitizo mkubwa sana.
 
“Jinsi unavyo endelea kupoteza muda kuwemo ndani ya hichi chumba ndivyo jinsi unavyo zidi kuiweka hali ya mgonjwa katika wakati mbaya zaidi. Tafadhali toka ndani ya chumba”
“Ni mama yangu”
“Ndio tunajua, ila acha tufanye kazi yetu Mr Ethan”
Mwanasheria akanishika mkono na taratibu akanitoa ndani ya chumba hichi.
“Nahitaji kuzungumza nawe”
Nilimuambia mwana sheria huku nikimtazama usoni mwake. Nikaanza kuondoka katika eneo hili pasipo kumuaga mtu yoyote. Tukafika katika kordo ya kuelekea katika eneo la chumba cha upasuaji.
“Ndio mkuu”
“Endapo mama yangu atakufa, nahitaji kumuua mtu mmoja baada ya mwengine walio husika katika hili jambo. Umenielewa?”
 
Nilizungumza kwa hasira huku nikimtazama mwana sheria usoni mwake.
“Sawa mkuu nimekuelewa”
“Ninaweza kuzungumza na vijana wako?”
“Si kwa muda huu muheshimiwa. Inabidi tuweze kukaa hapa tufahamu hali ya mama ina endeleeaje”
“Nalijua hilo, ila ninataka kuhakikisha kwamba nao wanapitia magumu kama magumu haya ambayo ninayapitia mimi kwa muda huu”
“Nimekuelewa muheshimiwa”
“Nitengenezee mfumo wa kuhakikisha kwamba ninamfahamu adui yangu mkuu na timu yake nzima aliyo shirikiana nayo”
“Sawa mkuu”
Nikarudi katika chumba cha kusubiria huduma, Camila akanisogelea karibu na sehemu niipo simama na akanishika kiuno changu.
“Kila kitu kinakwenda kuwa salama mume wangu sawa”
“Nashukuru”
Nilimjibu Camila kwa ufupi, akanibusu mdomoni mwangu na wala sikuweza kuwa na hisia za aina yoyote kwake. Baada ya masaa mawili na nusu mlango ukafunguliwa na akatoka daktari mkuu wa oparesheni hii. Watu wote tukasimama mbele yake huku tukimtazama usoi mwake.
“Poleni sana kwa kusubiria”
 
“Tunashukuru”
Mama Camila alijibu kwa kujiamini.
“Tunashukuru Mungu upasuaji umeenda vizuri, na tumefanikiwa kutoa damu iliyo kuwa imeganda kwenye ungong”
“Ohoo asante Mungu”
Mama Camila alijibu kwa unyenyekevu mkubwa sana.
“Sasa hivi tutamtoa mgonjwa humu na kumpeleka katika chumba cha wagonjwa mahututi. Humo atakaa kwa muda hadi pale hali yake itakapo kaa vizuri”
“Je anaweza kuzungumza?”
Nilimuuliza daktari huku nikimtazama usoni mwake.
“Hapana, kwa sasa hawezi kuzungumza, na kuna mambo kadhaa tutayazungumza ofisini, au kama nyote hapa ni wana familia basi ninaweza kuyazungumza sasa hivi?”
“Wewe zungumza tu dokta”
Nilitoa ruhusa hii kwa maana tuliopo hapa wote ni watu ambao ni msaada mkubwa sana kwangu.
“Kuna matatizo yamempata mama, nitayaeleza kwa hali ya kawaida tu na si kitaaamu sana.”
 
“Wewe zungumza tu daktari”
“Mama hato kuwana uwezo wa kukumbuka mambo yaliyo tokea na wala hato kuwa na uwezo wa kuona tena labda tu zitokee baraka za mwenyezi Mungu tu aweze kurudi katika hali ya kawaida”
Mwili mzimza ukazizima, nikahisi kunyong’onyea miguu yangu, mwana sheria akawahi kunishika kabla sijaanguka chini.  Kitanda alicho lazwa mama kikatolewa humu ndani huku kitanda hichi kikiwa kimezungukwa na manesi sita.
Tukaongozana na manesi hawa hadi kwenye chumba kimoja kikubwa, wakatuomba tuwasubirie waandae chumba hicho vizuri kisha sisi nasi tuingie kumtazama. Baada ya dakika kama kumi na tano tukaruhusiwa kuingia ndani ya chumba. Nikaingai peke yangu ndani ya chumba hichi na kumkuta mama akiwa anapumulia amshine huku nesi mmoja akiwa amesimama pembeni ya kitanda hicho. Machozi yakazidi kunibubujika nikiwa ninamuangalia mama yangu, hali yake kwa kweli ni mbaya sana. Mwili wake ume dhohofika na anaonekana ni mwana mama amabt maisha yake yalikuwa ni mabaya huko alipo kuwaa kiishi.
 
“Mama”
Niliita kwa sauti ya unyonge kiasi huku nikijaribu kumshika mama mkono. Mama hakuweza hata kupepesa jicho lake, machozi yakaendelea kububujika usoni mwangu, nesi alipo ona hali yangu inazidi kuwa mbaya akaniomba niweze kutoka ndani ya chumba hichi. Sikuweza kubisha maamuzi ya nesi huyu, nikatoka ndani ya chumba hichi huku nikiwa nimejawa na dukuduku kubwa sana moyoni mwangu. Wakaiingia watu wengine nilio ambatana nao mmoja baada ya mwengine kumuona mgonjwa. 
 
“Mungu atamsaidia mama atapona sawa mwanangu Ethan”
Mama Camila aliniambia mara baada ya kutoka katika chumba cha ICU.
“Sawa mama”
“Inabidi uende kula chakula sasa”
“Mama sijikii kula”
“Jitahidi tu mwanangu sawa”
“Sawa”
“Ethanm nitakwenda nyumbani na nitamueleza mama hili lililo jitokeza sawa mdogo wangu”
“Sawa dada”
“Hakikisha unapata chakula kama alivyo kueleza dada hapa”
“Poa poa”
Dada Mery akaniaga na kuondoka zake. Mwanasheria akaniita pembeni kwa ishara, nikamfwata.
“Vipi mkuu nikuandalie chumba katika hoteli ya hapa karibu?”
Nikaa kimya kwa muda huku nikifikiria cha kuzungumza.
“Nahitaji kukaa hapa”
 
“Sawa ngoja nikakutafutie chakula”
“Hapana, sihitaji chakula kwa sasa, nipo vizuri”
“Sawa mkuu basi naomba na mimi niweze kuelekea nyumba nikapumzike kidogo”
“Sawa wewe chukua muda wa kutosha pale nitakapo kuhitaji basi nitakufahamisha uweze kuja hapa”
“Sawa”
Mwanasheria na yeye akaondoka eneo hili na kuniacha nikiwa na Camila.
“Mume wangu naomba nikaongozane na walinzi nikachukue chakula kisha nirudi hapa, nitakuwa nawe na sinto kuacha peke yako sawa mume wangu”
“Sawa”
Camila akaninyonya midomo yangu kidogo kisha akaondoka katika eneo hili. Ethan mwenzangu akakaa pembeni yangu huku akinitazama usoni mwangu.
 
“Vipi mbona una huzuni sana?”
“Kwani hujui kilicho tokea Ethan?”
“Sikuhizi hunishirikishi mambo yako rafiki yangu, hadi pale utakapo kuwa na shida ndio una nikumbuka”
“Sio hivyo Ethan”
“Ila?”
“Kichwa changu hakikuwa vizuri kabisa”
“Sio hakikuwa vizuri rafiki yangu, kwa swala dogo kama hili kweli ulishindwa kunishirikisha mimi, hadi umeamua kutumia garama nyingi sana kwa vitu hivi?”
Ethan alizungumza kwa kulalamika.
“Samahani kwa hilo”
“Njoo nikuonyeshe kitu”
Ethan alizungumza huku akinyanyuka hapa pembeni yangu. Nikanyanyuka na tukaingia katika chumba cha alicho lazwa mama.
 
“Huyu ni nani yako?”
“Ethan aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Ni mama yangu?”
“Unaikumbuka sura ya mama yako vizuri?”
Swali la Ethan likanifanya nikae kimya kwa muda huku nikimtazama mama huyu.
“Hapana”       
“Kwa nini umeamini kwamba huyu ni mama yako?”
“Ethan, moyoni mwangu, ninahisi kabisa sura ya mama yangu”
“Acha ujinga Ethan, ni watu wangapi weusi ambao una fanana nao, unataka kusema kwamba ni ndugu zako. Hapa umechezewa mchezo wa ajabu. Sasa ni hivi huyu sio mama yako, mumepumbazwa na unapo pelekwa ni kufilisiwa kila kitu chako na utabambikiwa kesi ya mauaji umenielewa”
Maneno ya Ethan kidogo yakanifanya nishikwe na bumbuwazi huku nikimtazama usoni mwake, kwani haya anayo nieleza sijawahi kuyafikiria kabisa kwenye akili yangu.
                                                                                                       ITAENDELEA   


from MPEKUZI

Comments