Rais Dk John Magufuli amesema ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha anaitumia misaada inayotolewa na wafadhili ili ilete faida kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 27, alipokuwa akizindua maktaba mpya ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambayo imejengwa kwa ufadhili wa serikali ya China kupitia kampuni ya ujenzi Jiangsu Jiangdu kutoka nchini humo.
Maktaba hiyo ina majengo mawili, moja likiwa maktaba yenyewe na lingine ni la Tasisi ya Conficius ambayo itakuwa ikifundisha tamaduni za kichina kwa wanafunzi wa UDSM na watanzania wengine, ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kukaa watu 600, inahudumia wasomaji 2100 kwa wakati mmoja na kuhifadhi vitabu 800, 000.
“Nitashangaa sana kama siku moja nitapita hapa na kukuta ukuta umechorwa chorwa na makaratasi yamechanwa, maktaba hii itunzwe ili iwe ukumbusho kwa watanzania na wageni wanaokuja kututembelea lakini pia iwe kumbukumbu ya ushirikiano wetu na China, “ amesema.
Aidha pia Rais Magufuli ameipongeza Bodi ya ya Elimu ya Juu (HELSB) kwa kutoa mikopo kwa wakati ambapo asilimia 60 ya wanafunzi kwa mwaka wa kwanza ndio wamepata mikopo na kuwataka waendelee kufanya kazi kwa juhudi ili hao waliobaki wapate ziwasaidie kupata elimu yao.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment