Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Vicensia Shule ameitwa kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho kuhojiwa leo Ijumaa, Novemba 30, 2018 mchana kuhusiana na taarifa yake aliyoitoa kwenye mtandao wa Twitter akimuomba Rais Dkt. John Magufuli kuingilia kati kukithiri kwa rushwa ya ngono chuoni hapo.
Kupitia mtandao wa Twitter, Vicensia aliandika; "Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli."
Jana Alhamisi jioni aliandika kwenye Twitter kwamba amepigiwa simu na kutakiwa kufika mbele ya Kamati ya Maadili UDSM.
"Leo Alhamisi 29 Nov jioni nimepigiwa simu kuitwa kwenye Kamati ya Maadili siku ya Ijumaa 30 Nov mchana. Nasubiri mwaliko rasmi kwa maandishi.
"Kwa manusura wa udhalilishaji huu wa kingono, tunakaribia kufika, tutashinda, tutapata ushindi mkubwa!" Aliandika

Ingawa hakueleza ni rushwa ya aina gani iliyokithiri, lakini katika baadhi ya vyuo vikuu vingi kumekuwepo na tatizo la wahadhiri kuwarubuni wanafunzi kwa rushwa ya ngono ili wawafaulishe na pindi wanapogoma hupigwa sup, carryover.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment