Katibu Mkuu CCM Amtaka Zitto Kabwe Ahamie CCM

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amempongeza kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe kwa kuibua mijadala ya kiuchumi na kumkaribisha ajiunge na Chama chake cha CCM.

Akizungumza akiwa ziarani mkoani Iringa, Dkt. Bashiru amesema kuwa kiongozi huyo amekuwa akiibua mijadala mbalimbali ya kiuchumi na kumkaribisha kujiunga na chama hicho.

"Nampongeza kiongozi wa ACT-Wazalendo ndugu Zitto Kabwe kwa kuibua mijadala mbalimbali ya kiuchumi, nimtake na kumkaribisha ajiunge na CCM, chama cha ujamaa wa kweli", amesema Dkt Bashiru na kuongeza;

"Napenda kutumia hadhara hii kwa wote walioadhibiwa na wale waliosimamishwa uanachama milango ipo wazi kuomba msamaha na kusamehewa, tunajua walikosea ila hatutaendelea na visasi".

Katibu huyo ameongeza kuwa vyama vitakavyokufa kwenye uchaguzi ujao ni vyama vinavyoendeshwa kwa ajenda za matukio, vyama tegemezi vinavyotegemea mabepari, vyama vilivyochukua mafisadi na kuwaweka ngazi za juu.

"Hakuna mtu anayezuiliwa kugombea ila ni lazima afuate taratibu, atakayekiuka taratibu atakiona, baadhi wanatafuta Urais Zanzibar, wanapoteza muda Urais hauombwi, ni unaombwa. Hatuna urais wa udalali kwani ulipita toka mwaka 2015", ameongeza Dkt. Bashiru.


from MPEKUZI

Comments