Ray Kigosi Amvaa Wema Sepetu Sakata la Video Chafu Mitandaoni

Muigizaji Ray Kigosi amesema Wema Sepetu anapaswa kutumia mitandao kuingiza fedha na sio kufanya mambo ya hovyo.

Ray akizungumza na Wasafi TV amesema alichofanya Wema hakuna ambaye amefurahaishwa nacho hivyo kumtaka kubadilika.

"Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu atafurahia  yale matendo ambayo yamefanyika, huyo atakuwa ni tahira, una upungufu wa akili au atakuwa ni punguani," amesema Ray.

"Unamposti mpenzi wako mnakisi for what?, Wema ni brand kubwa abadilike asiwe na tabia ya kuomba msahaha na mambo yale yale yanajirudia atumie mitandao kuingiza pesa na sio kufanya upumbavu," ameeleza.

Hivi karibuni kulivuja video mtandao ya Wema Sepetu akiwa faragha na mtu ambaye aliwahi kutambulishwa kuwa ndiye mume wake mtarajiwa.


from MPEKUZI

Comments