Zoezi la Kuinasua MV Nyerere Lakamilika....Rais Magufuli Atoa Zawadi

Zoezi la kukinasua Kivuko cha MV Nyerere kilichopinduka Septemba 20 mwaka huu limekamilika baada ya kuvutwa hadi katika ufukwe wa kijiji cha Kisiwa Bwisya kisiwa cha Ukara.

Akitoa taarifa ya zoezi hilo, Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema michango ya maafa ya Kivuko cha MV Nyerere imefika Sh milioni 946 ambapo hadi sasa matumizi yamefika Sh milioni 266.

Kamwelwe amesema Rais John Magufuli ameagiza Sh240m zitatumika kuwapa asante waliohusika na uokoaji katika ajali ya MV Nyerere kila mmoja atapewa Sh 400, 000, zilizobaki zijenge mnara wa kumbukumbu, wodi ya akina mama, ya akina baba na ya watoto katika Kituo cha Afya cha Bwisya .

Aidha, Kamwelwe amesema leo  Jumamosi saa 7:00 mchana michango kwa ajili ya maafa ya kivuko cha MV Nyerere itasitishwa.


from MPEKUZI

Comments