RC Makonda Atuma Ombi Kwa Rais Magufuli

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli kufanya ziara ya mara kwa mara kwa Mkoa wa Dar es salaam ili kuwawezesha wananchi wa mkoa huo kumuona kiongozi huyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matumizi ya barabara ya juu Flyover Tazara jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amemuomba Rais Magufuli kuiongeza Dar es salaam kwenye ziara zake ili aweze kukutana na wananchi wa jiji hilo.

“Mheshimiwa Rais sina mengi ya kuomba kwako zaidi ya kukuomba unapofanya ziara zako mkoani uwe unakuja na Dar es salaam walau uwe unakutana na wananchi wa Mbagala, Yombo, pamoja na maeneo mengine maana hawa huwa wanakukumbuka sana, pia huwa tunaona wivu unapofanya ziara mikoani lakini kwetu hatukuoni.” Amesema Makonda

Aidha mkuu wa huyo mkoa ameeleza Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni linaingiza shilingi milioni 800 kwa mwezi kupitia tozo zinazotolewa na watumiaji wa daraja hilo pamoja na kueleza changomoto ya utapeliunaofanywa na baadhi ya madalali Dar es salaam kwa kushirikiana na taasisi za kifedha.


from MPEKUZI

Comments