Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mikono miwili ombi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda la kufanya ziara ya kikazi Mkoani humo ili kujionea miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano pamoja na kusalimiana na wananchi ambao wameonyesha kuwa na shauku kubwa ya kuonana na Rais.
Uamuzi huo umekuja baada ya RC Makonda kumuomba Rais Maguguli afanye ziara ya kikazi na kuzungumza na wananchi.
Hayo yote yamejiri leo wakati wa uzinduzi wa Flyover ya Mfugale iliyopo makutano ya TAZARA ambapo RC Makonda amempongeza Rais Magufuli kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo la aina yake linaloenda kumaliza kero ya Msongamano jijini Dar es salaam.
Aidha RC Makonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kukamilisha miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara za kisasa, Madaraja, mifereji, vituo vya afya, miradi ya maji na miradi mingine lukuki ambayo imekuwa faraja kwa wananchi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment