Msajili wa Vyama Awataka Viongozi wa Vyama Kuimarisha Demokrasia Ndani ya Vyama Vyao

 Vyama vya siasa hapa Nchini vimetakiwa kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao ili viweze kutekeleza majukumu yao kama taasisi imara tofauti na mawazo ya walio wengi kuwa vyama hivyo sio imara kiasi cha kufananishwa na vikundi vidogo vidogo katika Jamii kama vile Saccos.

Hayo yalisemwa na Msajili wa vyama vya siasa hapa Nchini Jaji Francis Mutungi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Viongozi wa Kitaifa wa vyama vya siasa jana  jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuvijengea vyama uwezo wa masuala ya rasimali fedha na rejista ya chama ili viweze kujiendesha kama taasisi.

Jaji Mtungi aliviambia vyama vya siasa kuwa ni muhimu kujenga vyama kama taasisi imara kwani mtu yeyote kutoka nje anayeitaji kuwekeza katika vyama hawezi kuwekeza katika chama ikiwa chama husika kitakuwa na hati chafu kutoka Ofisi yaMdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

‘’Mafunzo ya rasimali fedha na regista ya vyama kama vile mali za vyama ni muhimu kwasababu pamoja na vyama kupatiwa mafunzo haya ni vyema mkatambua kuwa vianawajibika kwa wananchi katika suala zima la utendaji wa ndio maana msajili analazimika kufanya ukaguzi katika vyama’’Alisema Jaji Mtungi.

Aidha Jaji Mtungi aliwaambia wawakilishi wa vyama vya siasa kuwa elimu ya fedha na regista ya chama ni muhimu kwasababu pia zoezi hili linasaidia sana kupunguza migogoro ndani ya vyama vya siasa.

Wakati huo huo Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mkandala ambaye aliwasilisha mada ya Jinsi ya Kuendesha chama kama taasisi,alisema lengo la chama cha siasa chochote ni kujiandaa kushika madaraka au kuwa wapinzani wa serikali hivyo lazima kuhakikisha vinajijenga kama taasisi inayoaminika kwa wananchi.

Profesa Mkandala alisema siasa vyama vingi hapa Nchini ni matokeo ya ukoloni mamboleo ambao ulianza kushamiri hapa nchini kwa miaka 1990 ambapo nchi ya Tanzania kama zilivyo nchi nyingine Barani Afrika zilikumbwa na mabadiliko ya kiuchumi ya soko huria ikiwemo nchi zilizokuwa za ujamaa kuanza kufuata m asharti ya Shirika la Fedha Duniani IMF.

Aidha Profesa Mkandala alitaja vigezo vinavyofanya chama kuwa Taasisi muhimu kuwa ni Itikadi, Uongozi bora, Wanachama, Sera na programu za chama, Rasilimali


from MPEKUZI

Comments