Msanii kutokea WCB, Mbosso amesema si sawa kwa yeye kufananishwa na Aslay.
Muimbaji huyo akizungumza na Waandishi kwenye red carpet ya Biko Jibebe Challenge amesema kuwa Aslay ameenza muziki muda mrefu kuliko yeye, hivyo si sawa kuwashindanisha.
"Hakuna kitu ambacho najisikia vibaya mara kwa mara kama kuona nashindanishwa na Aslay, ni brother yangu, na isitoshe mimi nimeanza muziki kama solo artist nina miezi tisa tu. Aslay kaanza 2011 kwa hiyo ni mkubwa sana kwangu, mimi bado mchanga mno, ukinifananisha naye unamvunjia heshima yake," amesema Mbosso.
Aslay alianza kusikika kimuziki kabla ya kuundwa kwa kundi la Yamoto Band ambalo alikuwepo pia na wasanii wengine kama Mbosso, Beka Flavour na Enock Bella.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment