Korea Kaskazini: Hatutaharibu silaha zetu ikiwa vikwazo vya Marekani vitaendelea kuwepo

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini ameonya kwa kusema kuwa nchi yake haiwezi kuharibu zana za nyuklia wakati Marekani bado inaendelea kuiwekea vikwazo.

Ri Yong-ho aliuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuwa vikwazo hivo vinapunguza imani yake kwa Marekani.

Hivi karibuni Korea Kaskazini imerejelea wito wake wa kuitaka Marekani na Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo na imeungwa mkono kutoka China na Urusi.

Lakini uongozi wa Trump unasema kuwa vikwazo hivi vitadumu hadi pale Korea Kaskazini itakapoharibu zana zake za nyuklia.

"Bila ya imani kwa Marekani hatuwezi kuwa na uhakika kwa usalama wetu wa kitaifa na katika hali kama hiyo hakuna vile tutaharibu silaha zetu kwanza." alisema Ri

"Imani kuwa vikwazo vinaweza kuchangia sisi kusalimu amri ni ndoto," aliongeza.

Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walifanya mkutano wa kihistoria mwezi Juni huko Singapore ambapo Bw Kim aliahidi kuharibu zana za nyuklia.
 
Makubaliano yaliyoafikiwa huko yalisema kuwa Korea Kaskazini ingeharibu zana zake za nyuklia lakini hayakuwa na mwongozo au muda au njia kuthibitisha mchakato huo.

Mwezi Agosti Rais Trump aliilaumu China ambaye ni mshirika wa Korea Kaskazini kwa suala hilo kutokana na tofauti zake za kibiashara na Marekani.


from MPEKUZI

Comments