Dereva wa bodaboda, Aman Mika (22) amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba(14).
Akisoma shtaka hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Frank Moshi, Wakili wa Serikali, Ramadhani Mkimbu alidai tarehe tofauti mwaka 2017 hadi Agosti maeneo ya Mbweni mshtakiwa alimbaka mwanafunzi huyo.
Mkimbu alidai mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo huku akijua kubaka ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo alimuomba hakimu apange tarehe ya kutajwa.
Hakimu Moshi alimweleza mshtakiwa kuwa dhamana yake iko wazi kwa kuwa shtaka linalomkabili linadhaminika.
Moshi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja awe na barua inayotambulika na asaini bondi ya Sh500,000.
"Kwa kuwa umeshindwa masharti ya dhamana unaenda mahabusu hadi Oktoba 11 mwaka huu kesi yako itakapotajwa tena,"alisema Hakimu Moshi

from MPEKUZI
Comments
Post a Comment