Serikali Yakaa Ombi la Wadau Kuhusu Kuondolewa kwa Channel za Channel Ten, ITV, Star Tv, EATV na Clouds Tv

SERIKALI imewataka watoa huduma wa ving’amuzi vya Azam, Multichoice na Zuku wazingatie sheria na kanuni kwa kutorusha maudhui ya televisheni ambayo hayamo kwenye leseni zao za biashara.

Hatua hiyo ya serikali imekuja baada ya huduma za utangazaji wa maudhui za Channel Ten, ITV, Star Tv, EATV na Clouds Tv kusitishwa kwenye king’amuzi cha Azam kwa mujibu wa tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) la Agosti 7, mwaka huu.

TCRA ilitangaza hivi karibuni kupitia vyombo vya habari kusudio la kuzifunga leseni za kampuni ya Multichoice, Zuku na Azam endapo wataendelea kuonesha maudhui ya chaneli hizo za televisheni kwa watazamaji kwa vile ni kinyume cha sheria na kanuni za leseni zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema Agosti 11 mwaka huu, vituo vya ITV, Clouds Tv, EATV na Channel Ten walitoa tamko lao kupitia mitandao ya kijamii vikitaka busara iliyotumika awali kwa vituo hivyo kupeleka maudhui yao kupitia ving’amuzi vya Zuku, Azam na Multichoice kinyume na sheria, iendelee wakati utaratibu wa kurekebisha hali hiyo ukiendelea.

Kamwelwe alisema hoja hiyo imepingwa na serikali kwa kuwa TCRA haiwezi kukaa kimya huku sheria na kanuni za utangazaji zikivunjwa na watoa huduma hao.

“Watoa huduma hao Azam, Multichoice na Zuku waliamua kwenda Mahakama Kuu kupinga maamuzi ya TCRA, lakini Mahakama Kuu ilitupilia mbali pingamizi hilo la Agosti 22, 2017,” alieleza Kamwelwe.

Kwa mujibu wa Kamwelwe, leseni namba moja ya vituo vya televisheni nchini inawataka kutoa matangazo yao ikiwemo habari, sherehe za kitaifa, matukio ya magonjwa, vipindi vya watoto na sherehe za kitaifa bure bila kuwataka wananchi kulipia huduma hizo.

Amesema huduma binafsi kama vile mchezo wa mpira kwenye nchi za nje pamoja na tamthiliya ni michezo binafsi ambayo mwananchi kwa ridhaa yake anaweza kulipia ili aone.

Baada ya kadhia hiyo, Kamwelwe alisema endapo watoa huduma hao, hawataendelea kutoa huduma wanazotakiwa kisheria kwa mujibu wa leseni zao, serikali itato tamko la kuwataka wawafidie wananchi ambao ni wateja wao


from MPEKUZI

Comments