Madiwani Watano wa CHADEMA, CUF Watimkia CCM

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Madiwani watano wa vyama vya upinzani ikiwemo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, CUF na ACT Mzalendo na viongozi wengine sita wamevikimbia vyama hivyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani.
 
Madiwani hao ni pamoja na Ramadhan Lutambi aliyekuwa diwani wa kata ya Mailmoja kupitia Chadema na Ramadhan Kombe aliyekuwa diwani  kata Mbwawa kupitia ACT. 
 
Wengine ni, Muharami Mkopi Cuf kata ya Ruaruke wilayani Kibiti,Seif Lwambo kupitia Cuf kata ya Beta,Muharami Mketo Cuf Kata ya Lukanga na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukanga.
 
Aidha viongozi waliojiuzulu kwenye vyama hivyo ni Ayubu Chapile ambae alikuwa katibu kata ya Mkuza (CUF) ,Karimu Kasimu katibu tawi chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere (Chadema) ,Selemani Mwinyimkuu mwenyekiti tawi (Cuf),David Mramba Act,Latifa Sangalala mwanachama Chadema Mkoani B na Jumanne Urembo Diwani kivuli ACT kata ya Sofu.
 
Awali Ramadhani Lutambi alisema ,chama kinachofaa kuongoza nchi daima ni CCM kwani vyama vingine havina uwezo,na havijali  viongozi wa ngazi za chini .
 
Alifafanua ,ameamua kuondoka Chadema ili kutekeleza yale yanayofanywa na Rais Dk. Magufuli kwa wananchi wanyonge.
 
Lutambi alikiri kuondoka Chadema kwa hiari yake, kwa akili zake timamu na kudai anajivua vyeo vyote alivyonavyo kuanzia sasa. 
 
Akiwapokea madiwani na viongozi wa vyama hivyo kwenye ofisi za CCM Mkoa, mwenyekiti wa CCM mkoani Pwani, Ramadhani Maneno alisema ,kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani wameona hakuna sababu ya kubaki kwenye vyama vyao.
 
Alisema kazi kubwa inayofanywa na chama kupitia Rais Dk .John Magufuli ndio sababu kubwa ya madiwani na viongozi hao kukimbilia CCM. 
 
“Baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha kuwa wabunge,madiwani na viongozi wanaohamia CCM wananunuliwa ,suala hili halipo ,ni kwamba wanarudi kutokana na utendaji kazi wa chama chetu,” alisema Maneno.
 
Maneno alieleza, viongozi hao hawanunuliwi wala kuhongwa bali ni mapenzi yao .
 
“Kuhusu gharama za uchaguzi kuwa ni kubwa hilo ni suala la Tume ya uchaguzi na chama kisilaumiwe kwani kuhama kwao hakuhusiani na kurubuniwa ,” alisema Maneno.


from MPEKUZI

Comments