Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewatoa nje Makamanda zaidi ya 30 kwa kosa la kutaja Jeshi la Zimamoto bila kumalizia ‘na Uokoaji’ ambapo amesema hilo jeshi lao halitambui.
Hali hiyo imejitokeza leo Alhamisi Agozti 30, jijini Dodoma kwenye ufunguzi wa kikao cha mwaka cha Makamanda wa Zimamoto na Uokoaji ambapo amesema makamanda hao wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea.
“Mimi nalijua Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wale wote ambao walijitambulisha bila kumalizia na uokoaji watoke nje.
“Nisikilizeni kwa makini makamanda ambao nimewaita majina yenu simameni na ambao hamjasikia nikitaja majina yenu tokeni nje kwani hilo jeshi lenu mlilolitaja silitambui hivyo kikao hiki hakiwahusu.
“Haiwezekani ofisa mzima unasimama unajitambulisha kuwa unatoka Jeshi la Zimamoto, kwa hiyo kazi yenu nyinyi ni kuzima moto tu na siyo pamoja na uokoaji,” amesema.
Waziri Lugola alisema amefanya hivyo kwa kuwa anataka jeshi hilo lijitambue kuwa ni jeshi lenye majukumu hayo kwani lipo na lilianzishwa kwa mujibu wa sheria kuwa ni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Hata hivyo, Lugola baada ya kuwatoa nje makamanda hao aliwaruhusu kuingia kushiriki kikao hicho wakiwa kama wageni waalikwa na si wahusika wa kikao hicho.
Maofisa wa Jeshi la Zimamoto wakitoka nje baada ya kutolewa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment