Jenerali Davis Mwamunyange ateuliwa kwenye tume ya kuchunguza ghasia za baada ya uchaguzi Zimbabwe

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnagangwa amteua Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange katika Tume ya Kutathmini athari za ghasia zilizotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Katika tume hiyo yumo aliyewahi kuwa Rais wa Afrika Kusini (Septemba 2008 hadi Mei 2009), Kgalema Petrus Motlanthe pamoja na waharidhiri na wanadiplomasia kutoka Nigeria na Uingereza.

Ghasia katika uchaguzi uliofanyika Julai 30 zilisababisha vifo vya watu 6 na wengine wakiwa wamejeruhiwa.


from MPEKUZI

Comments