Kuna taarifa kuwa msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Mr. Nice amekwama Kampala Uganda baaada ya promota Abtex wa Abtex Promotion kushindwa kumlipa fedha msanii huyo ambaye walikubaliana kuwa angetumbuiza kwenye tamasha la Ekyeppukulu, June 24, 2018 kwenye uwanja wa Namboole
Kutoka wakati huo (mwezi Juni) kumekuwa na uvumi kuwa Mr. Nice amekwama Kampala baada ya Abtex kushindwa kumlipa fedha zake.
Taarifa zinaeleza kuwa Mr. Nice alifikia kwenye hotel Sport View ndani ya Kirenga ambapo alikaa hapo kwa siku kadhaa kwa ajili ya tamasha hilo, hata hivyo taarifa nyingine zinadai kuwa muimbaji huyo kabaki Kampala kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.
Hata hivyo pia katika video iliyowafikia Mseto East Africa, Mr. Nice alijibu yote yanayozungumzwa kuhusu yeye kukwama Kampala.
"Kuna uvumi kwamba Mr. Nice amekwama Kampala, ninaweza kukwama kwenye eneo langu? Abtex hakunilipa hata asilimia moja. Huyu jamaa alipotea kabisa na nilipata mateso lakini Mr. Nice ni jina kubwa hivyo nikajitenga kwenye hali hiyo mwenyewe, haikuwa vizuri kwa wao kunifanyia hivi" amesema.
Ili kuthibitisha zaidi kwamba wanaomkosoa/kumbeza kuhusu hilo hawapo sahihi, Mr. Nice alionyesha gari aina Range Rover 2018 ambayo anaendesha kila siku akifurahia maisha Uganda huku bado akiendelea kuishi kwenye Hotel.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment