DC Jokate Mwegelo, Hamisa Mobeto Wateuliwa Kuwa Mabalozi wa Kampeni ya BE SMART. ya TCRA

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo,mwanamitindo Hamisa Mobeto, wanamuziki Barnaba , Shilole na muigizaji wa vichekesho Dullvani wamechaguliwa kuwa mabalozi wa  kampeni maalumu inayohusu elimu kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii iliyopewa jina la BE SMART.

Kampeni hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA CCC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kuanza Septemba 3 katika shule za sekondari.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu na Mwanzilishi wa kampeni hiyo, Marry Msuya alisema wasanii hao wamechaguliwa kuwa mabalozi kutokana  na michango yao kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii.

“Wasanii hawa wamekua wakitumia mitandao katika mambo mbalimbali ya kujinufaisha wengine wanatangaza biashara na wengine wanaonyesha vipaji mbalimbali walivyonavyo”. Amesema katibu huyo.


from MPEKUZI

Comments