BREAKING: Rais Magufuli Apigilia Msumari Sakata la Makontena ya Makonda....Asema Ni Lazima Yalipiwe Kodi

Rais John Magufuli amewataka viongozi kujenga mazingira ya kuwatumikia wananchi bila kujali wapo kwenye nafasi gani.

Magufuli ameyasema hayo leo Agosti 30, akizungumza na madiwani, viongozi na watumishi wa Halamshauri ya Wilaya ya Chato, Geita.

Akizungumza katika Mkutano uliofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Magufuli ametolea mfano sakata la makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yanayotarajia kupigwa mnada baada ya kushindwa kulipiwa kodi bandarini.

“Umesikia hili sakata la Dar es Salaam, eti Mkuu wa Mkoa, ameleta makontena, ameambiwa alipe kodi, kwa nini asilipe kodi?” amesema.

 Amesema sheria za nchi zinasema wazi kuwa ni mtu mmoja tu katika nchi mwenye dhamana ya kutolipa kodi kwa mujibu wa sheria ya fedha, sheria ya madeni, sheria ya dhamana na ya misaada.

 Rais Magufuli aliitaja sheria hiyo kuwa ni namba 30 ya 1974, kifungu cha 3, 6, 13 na cha 15 ndicho kinampa mtu huyo dhamana ya kupokea misaada. Rais Magufuli amesisitiza. “Hakuna mtu mwingine.”

 “Sasa ukichukua makontena kule, umezungumza na watu wengine labda na wafanyabiashara, unasema ni makontena yako,  halafu ukasema tena labda ni ya  walimu, wala hata shule hazitajwi,  Maana yake nini?”

“Maana yake si unataka utumie walimu, ulete haya makontena, utapeleka  shule mbili au tatu, ndizo zitapewa mengine unakwenda kuyauza unapeleka kwenye shoping mall. Lakini walimu walikuambia wanahitaji makochi, sofa,” amesema.

Rais Magufuli aliwataka wafanyakazi wasitumike kwa maslahi ya watu fulani.


from MPEKUZI

Comments