Shirika la ndege Tanzania (ATCL), jana Agosti 30, 2018 limeanza safari yake ya pili ya nje ya nchi ikielekea Bujumbura, Burundi.
Safari hiyo ilianza jana asubuhi saa 3 kamili ambapo ndege aina ya Bombadier Q400, iling’oa nanga uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Dar es Saalam.
Taarifa iliyotolewa Agosti 30 na Kitengo cha Habari na Maelezo cha Waziri Mkuu, imeeleza kuwa hiyo inakuwa ni safari ya pili ya nje ya nchi baada ya ile ya Agosti 26 ambapo ndege hiyo ilielekea Entebe, Uganda.
“Kuanza kwa safari hiyo mpya ya Bujumbura kutafungua milango ya kibiashara na kitalii baina ya Tanzania na Burundi, pia kutaongeza wigo wa safari za ndege za shirika hilo linalofufuliwa,” imesema taarifa hiyo
Akipokea ndege kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreaamliner, Julai mwaka huu, Rais John Magufuli alisema nchi inang’aa na imefunguka kimataifa kwani uwezo upo na nia ya kuona shirika la ndege la Tanzania linaimairika, nayo ipo.
Alilitaka shirika hilo kubuni mikakati ya kibiashara ambayo itawawezesha kudumu kwenye ushindani lakini pia kupata faida ya kutosha na hatimaye kutoa gawio kwa serikali.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment