Viongozi Wapya Walioteuliwa na Rais Magufuli Wataapishwa Kesho.....Wakuu wa Mikoa Yote Wametakiwa Kuhudhuria Tukio Hilo
Rais John Magufuli Jumatano Agusti 1, 2018 atawaapisha viongozi mbalimbali aliowateua Jumamosi iliyopita.
Taarifa iliyotolewa jana Julai 30, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema viongozi hao ni, wakuu wa mikoa wanne na makatibu wakuu wawili.
Wengine ni, naibu makatibu wakuu wawili na makatibu tawala wa mikoa 13.
“Wakuu wa mikoa yote ya Tanzania Bara mnapaswa kuhudhuria tukio hili,” imeeleza taarifa hiyo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment