Muleba Kuunganishwa Umeme Gridi Ya Taifa

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), lipo mbioni kuiunganisha Wilaya ya Muleba mkoani Kagera na umeme wa gridi ya Taifa ili kuvutia wawekezaji hasa katika sekta ya viwanda nchini.

Akizungumza jana wakati wa shughuli ya kuunganishaji wa laini ya umeme wa gridi ya Taifa inayofanyika katika vijiji ya Kitete Wilayani Chato Mkoani Geita, Meneja wa Tanesco Wilaya ya Muleba, Julius Bagasheki, amesema kazi ya uunganishaji wa umeme wa gridi ni utekezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama tawala CCM kwa kuhakikisha wanatekeleza sera ya Tanzania ya Viwanda.

Alisema umeme huo wa gridi kwa Wilaya ya Muleba tayari wameanza na mradi wa uunganishaji 33KV ambao sasa unakwenda kuifanya Muleba kuwa na umeme wa uhakika.

“Umeme wetu tunachukulia kutoka Uganda ila ila kwa mradi huu sasa unakwenda kuifanya Wilaya ya Muleba kuwa na umeme wa uhakika wa gridi wa Taifa ambao haukatiki ovyo.

“Sisi Tanesco Muleba na Mkoa wa Kagera kwa ujumla tumejipanga vema kuitekeleza kwa vitendo sera ya Tanzania ya viwanda. Hivyo tunawaalika wawekezaji mbalimbali hasa wa sekta ya viwanda sasa waje Muleba kujenga viwanda kwani muda si mrefu tunakwenda kuwa na umeme  wa uhakika wa gridi ya Taifa ambao ni mkombozi wa uhakika,” alisema Bagasheki

Baadhi ya wananchi ambao wameshafikiwa wa umeme wa REA III, katika Kijiji cha Kitete, wamesema kuwa hatua ya kupata huduma hiyo sasa wanakwenda kupata maendeleo ya kasi ya kuweza kujiletea maendeleo kwa kuwa na uhakika wa umeme.

Mmoja wa wananchi hao Veronica John, ambaye ni mmiliki wa Duka la Dawa Muhimu (DLDM) ameishukuru serikali kwa kuwafikishia huduma ya umeme kwenye kijiji chato.

“Zamani tulikuwa tunanunua mafuta ya taa kwa gharama kubwa lakini baada ya serikali tuletea umeme nasi sasa tutapata maendeleo.  Hivi karibuni nitatununua jokofu kwa ajili ya kuhifadhi dawa ili zisiweze kuharibika baada ya kupata umeme. Kwa kweli tuna furaha ya hali ya juu,” amesema Monica

Naye Kinyozi Makoye Mwango, amesema kuwa hatua ya kupata umeme imemsadia kutoa huduma ya uhakika kwa wateja wao ambao hufika kunyoa nywele kwa uhakika.

“Awali tulikuwa tunachaji betri kwa gharama kubwa na unanyoawateja wawili hadi watatu… kwa sasa baada ya umeme kuja kwa kweli ninaweza kunyoa watu wengi za zaidi na kipato changu kimeongezeka mara dufu, hongera serikali pamoja na Tanesco,” amesema Mwango.


from MPEKUZI

Comments