Mkurugenzi wa halmashauri ya Mtwara, Omari Kipanga, amekiri kupata nakala ya barua ya kujitoa kwa Mgombea wa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Muungano, halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Mkurugenzi huyo amepokea barua hiyo ya mgombea udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Ismail Liuye jana ikiwa ni siku chache zimesalia kabla ya kufikia uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu.
Taarifa zinaeleza kuwa Bw. Liuye amejitoa katika kinyang'anyiro hicho baada ya kupokea vitisho kwa kutoka kwa watu mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi, akitishiwa maisha yake pamoja na familia yake.
Hata hivyo baada ya kuzungumza na bwana Liuye amedai kwamba ameamua kuacha kutokana na kwamba ni uamuzi wake.
"Mimi siendelei na kampeni, nimeacha. Nimeacha tu. Mtu unapoamua kuacha kitu si unaacha tu. Sababu nilizonazo ni za kwangu binafsi. Kama inasemekana kuhusu kutishiwa iendelee kusemekana".Amesema
"Mimi siendelei na kampeni, nimeacha. Nimeacha tu. Mtu unapoamua kuacha kitu si unaacha tu. Sababu nilizonazo ni za kwangu binafsi. Kama inasemekana kuhusu kutishiwa iendelee kusemekana".Amesema
Hata hivyo Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema kwa sasa bado hana taarifa za kuhusu kujiondoa kwa mgombea wao katika kinyang'anyiro hicho na kwamba anachoamini kampeni zilikuwa zikiendelea labda awe amejiondoa baada ya Kampeni za jana na kwamba bado anafuatilia habari hizo.
Pamoja na hayo Mkurugenzi Kipanga ameeleza kutokana na muda wa kuweka wagombea kupita, mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM, Hassan Likuto, atapita bila kupingwa kutokana na kutokuwapo kwa mgombea wa Chama kingine hivyo wanachosubiri ni taratibu za Tume waweze kumtangaza Likuto.
Hata hivyo amesema uchaguzi bado unaendelea katika Kata nyingine mbili zilizosalia.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment