Lugola Amtumbua Inspeka Mwingine wa Polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemvua ujumbe wa Sekretarieti ya Kuzuia Biashara Haramu ya Binadamu, Abubakar Yunusi ambaye ni Inspekta wa Polisi Kitengo cha Uhamiaji.

Lugola amechukua uamuzi huo leo Julai 30, 2018 wakati akikagua mabanda ya maonyesho katika viwanja vya mnazi mmoja yanapofanyika  maadhimisho ya kupinga usafirishaji wa bindamu, ambapo Yunusi amesema kuna vyombo vilivyotumika kusafirisha binadamu vimekamatwa na vinasubiri kutaifishwa, lakini hana idadi ya vyombo hivyo.

“Unafanya kazi ya ubabaishaji hapa? huwezi kuja kwenye maonyesho hujui idadi yake,kazi yako ya ujumbe hakuna, wewe umejitambulisha mjumbe wa kamati ya kudhibiti usafirishwaji haramu wa binadamu, umesema kuna vyombo vimetumika,lakini  huna idadi yake”, amesema Lugola.

Inspekta Yunusi anakuwa mtu wa tatu kuvuliwa madaraka na Waziri Lugola tangu alipoingia madarakani, ambapo Julai 6, 2018 katika mkutano wake na wanahabari aliagiza kushushwa vyeo kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya, Leopold Fungu na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Kagera, George Mrutu.


from MPEKUZI

Comments