Lugola Ampa Miezi Minne Lugumi....Akishindwa Atamtupa Mahakama ya Mafisadi

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ametoa onyo kwa mfanyabiashara  Said Lugumi baada ya kumpa miezi minne ya kukamilisha makubaliano  ya mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani, jijini Dar es Salaam jana Jumanne Julai 31, 2018 Waziri Lugola alisema kuwa mahakama  ya  kushughulikia kesi za rushwa iliyoanzishwa na Rais Dkt.Magufuli  bado haijapata wateja wakati ni wengi wanaoiba fedha za serikali.

“Mahakama ya kushughulikia kesi za rushwa inakosa wateja,na wanaoibia serikali wapo wengi mtaani,na kutokana hili  Saidi Lugumi nimempa miezi minne kukamilisha makubaliano ya mkataba na akishindwa atakuwa mteja wa mahakama hiyo” amasema Lugola.

Aidha Waziri Lugola aliongeza kuwa  mkataba unaomhusu mfanyabiahashara Said Lugumi  bado unafanyiwa uchunguzi na taasisi ya  kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) na baada ya uchunguzi hatua sitahiki zitachukuliwa.

Ikumbukwe kuwa mfanyabishara huyo aliingia katika msuguano na serikali mwaka 2016, ambapo kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) ilibaini ubadhilifu katika mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Jeshi la Polisi chini ya Mkuu wa jeshi la polisi wakati huo Ernest Mangu.

Mkataba huo  ulisainiwa kwa ajili ya  kufungwa  kwa mashine za utambuzi wa alama za vidole (AFIS) kwenye vituo 108 kwa gharama  ya shilingi bilioni 37 ambapo kampuni hiyo ilifunga  mashine hizo kwenye vituo 14 tu.


from MPEKUZI

Comments