Kauli ya Ndugai baada ya Waitara kujiuzulu

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema amepokea barua kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara ya kujivua uanachama wa Chadema na kujiuzulu wadhifa huo.

Ndugai amesema hayo leo Jumatatu, Julai 30 akiwa Ikulu jijini Dar  wakati wa hafla ya Rais John Magufuli kutoa hati za viwanja vilivyopo Dodoma kwa mabalozi 62 wa nchi mbalimbali na mashirika matano ya kimataifa kwa ajili ya kujenga ofisi na makazi.

“Kwa kuwa nimeambiwa ninaonekana nchi nzima, napenda nitangaze kuwa leo asubuhi nimepokea barua kutoka kwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kuwa amejivua uanachama wa chama chake na kujiuzulu ubunge’ amesema Ndugai ambaye alikaribishwa kutoa salamu kutoka Dodoma.

Ameongeza ataiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili taratibu zifuate.

“Kilichobakia ni kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa rasmi jimbo la Ukonga liko wazi’ ameseam Ndugai.

Waitara alitangaza kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM Jumamosi iliyopita.


from MPEKUZI

Comments