Na Magreth Kinabo
Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe .Profesa Ibrahim Juma amewataka mahakimu wapya wasiwe chanzo cha ucheleweshaji wa mashauri.
Aidha kuacha kulalamika bali pale linapotokea matatizo, bali wawe chachu ya kuyatafutia ufumbuzi katika utendaji wao wa kazi wa kutoa huduma za haki kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana na Jaji Mkuu huyo wakati akiwaapisha Mahakimu wapya kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
“ Kiapo mlichoapa ni uzito muda wote mtakaofanya kazi ya kuwatumikia wananchi, wananchi wanataka kutatuliwa kwa malalamiko yao kwa haraka,”
Aliongeza kwamba mfumo wa sasa sio wa kukaa na kulalamika, kama kuna tatizo litafutiwe ufumbuzi na kuepuka kuwa chanzo cha ulalamishi.
Alisema mahakimu hao wanapaswa kuwa weledi wanapotoa huduma za utoaji haki ili waweze kutoa hukumu zinazoeleweka kwa kujibu wa sheria na kanuni. Hivyo wanapaswa kushirikiana na wadau wengine wa mahakama ili kuahakikisha hukumu zinatoka kwa haraka.
Alisisitiza mahakimu hao kwamba kufanya kazi kwa kuepuka rushwa na kwa nidhamu.
Jaji Mkuu huyo alifafanua kuwa changamoto za majengo chakavu na umbali , visikwamishe utendaji kazi wao, hivyo mahakama iko katika Mpango Mkakati wa Miaka Mitano ambao unalenga kutoa huduma za haki kwa wote na wakati, ikiwemo kuboresha miundombinu.
Aliwataka mahakimu hao kuielewa taasisi inayofanyakazi na mpango mkakati huo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment