Dreamliner Yatua kwa mara ya kwanza Mwanza na Kupokelewa Kwa Heshima Kubwa

Wakuu  wa mikoa sita jana, walikuwa miongoni mwa wageni walioipokea ndege mpya aina ya Boeing 787-8 kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mangola wakuu wa mikoa walishuhudia ndege hiyo ya kisasa, ikitua kwa mara ya kwanza mjini hapa saa 4:19 asubuhi ikiwa na abiria 255.

Wakuu wa mikoa hiyo, Adam Malima (Mara), Mhandisi Robert Gabriel (Geita), Zainabu Tarack (Shinyanga), Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu (Kagera) na na Anthony Mtaka (Simiyu) na viongozi dini

Akizungumza wakati wa mapokezi ya ndege hiyo,Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele alisema Serikali ina mpango wa kuboresha majengo ya abiria na mizigo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa viwanja vya ndege nchini.

Alisema baada ya kuanza upanuzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,Uwanja wa Ndege wa Songwe, sasa wametenga fedha kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Mwanza.

Alisema uwanja wa Mwanza ndiyo mrefu kuliko viwanja vyote, ukiwa na urefu wa kilomita 3.9, kubainisha kwamba ujio wa ndege mpya aina ya Boeing 787-8 (Dreamliner) utakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na maendeleo.

Naye Mongela alisema safari ya Mwanza kwenda Dar es Salaam kupitia Kilimanjaro kwa ndege, ni muhimu hivyo huduma ujio wa ndege ni muhimu sana kwa wakazi wa Mwanza na mikoa jirani.


from MPEKUZI

Comments