Ziara Ya Ujumbe Wa Idara Ya Maadili Na Nidhamu Ya Chama Tawala Cha Frelimo Kutoka Msumbiji Ilipotembelea CCM Arusha.
Jana tar. 13 Juni, 2018 Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha imekutana na Ujumbe wa Idara ya Maadili & Nidhamu ya Chama Tawala cha FRELIMO Kutoka Nchini Msumbiji.
Ujumbe huo uliongozwa na Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu na Gavana wa Jimbo la Mkoa wa Maputo Nchini Msumbiji Mh. Raimundo Maico Diomba Umekutana na Uongozi wa CCM Mkoa wa Arusha mapema jana Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha ili kujifunza mambo kadha wa kadha ikiwemo ni jinsi gani CCM inaweza kusimamia na kuongoza Vikao vya ngazi mbalimbali kwa nyakati mbalimbali pindi kiongozi ama mwanachama anapokwenda kinyume na maadili ya Chama.
“Ama kwa hakika tumejifunza mengi na kubadirishana mawazo jinsi ya kuboresha Vyama vyetu viendelee kufanya vizuri kwa Wananchi wake ikiwemo kusimamia vyema Maadili kwa wanachama na Viongozi wake
"Nimependa sana Katiba ya chama cha FRELIMO inayomtambua Mkuu wa Mkoa kama Katibu Msaidizi wa FRELIMO Mkoa husika lakini pia Katiba ya nchi yao inasema baada ya Uchaguzi Mkuu ilani inayotekelezwa ni ya Chama kilichoshinda nafasi ya Urais," Alisema Robert Kaseko ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha na kuongeza kuwa;" Urafiki wetu na ndugu zetu FRELIMO daima utaendelea Kulindwa kwa nguvu zote."
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment