Victoria Kimani Adai Ana Mwaka Mzima Hamju Mwanaume

Msanii mkali kutoka Kenya mwanadada Victoria Kimambi amefunguka na kuweka wazi kuwa amepitisha mwaka mzima bila kukutana kimwili na mwanaume yoyote.

Victoria amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameweka wazi kuwa anasumbuliwa na upweke ambao umesababisha Kupitiasha takribani mwaka mzima bila kufanya mapenzi

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Victoria ameweka kipande cha wimbo chenye maandishi kilochosomeka:

"Huu ni mwezi gani tupo nao? Tangu Mei mwaka jana sija-du na mwanaume yeyote. Kwa hiyo nani ameshindwa? Ni mimi? Au ni wanaume. Ni ngumu. Ni kama tupo kwenye ongezeko la joto duniani”.

Victoria ambaye ameweka makazi yake nchini Nigeria ambapo anafanya kazi zake za kimuziki amekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na  producer wa video nchini humo ambaye Mahusiano yao yaliisha tangu mwaka jana May.


from MPEKUZI

Comments