Tundu Lissu Afunguka Mazito Kuhusu Dereva wake na Mwenyekiti Freeman Mbowe

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameamua kuondoa utata kutokana na kile ambacho kimekuwa kikihojiwa na baadhi ya watu kuhusu shambulio alilopitia Septemba 7, 2017 Area D huko mkoani Dodoma.
 
Mbunge huyo amesema kwamba mara nyingi hapendi kujibizana na watu wanaohisi kwamba maswali kuhusu shambulio lake yanaweza kukosa majibu kutoka kwa viongozi wa chama chake ambapo amesema yeye kama muathirika na kiongozi wa CHADEMA atatoa ufafanuzi.

Lissu amewajibu wanaotaka kumvisha dereva wake uhusika wa shambulio lake hasa baada ya kutofika kituo cha polisi kuhojiwa, amesema kuwa utaratibu wa kisheria haukufuatwa na baada ya shambulio hakukuwa na wito wa kumtaka yeye (dereva) afike kituo cha polisi mpaka alipofika Nairobi.

"Dereva wangu aliondokea Dodoma kuja Nairobi na aliletwa na Mheshimiwa Goddie Lema. Hakukuwa na wito wowote kutoka polisi ambao hakuutii. Polisi walipoanza kuulizia habari zake tuliwaambie wamfuate Nairobi alikokuwa. Tuliwaambia wafuate utaratibu wa Sheria ya Kusaidiana Katika Masuala ya Jinai ili dereva wangu na mimi mwenyewe tuhojiwe kuhusiana na shambulio dhidi yangu.  Waliahidi kuja Nairobi. Tuliwasubiri, hawakuonekana mpaka tuliposafiri kuja Ubelgiji" Lissu.

Ameongeza kuwa dereva wake alisafiri kwenda Ubelgiji kwa pesa zile zile za msaada wa Wasamaria wema.

Akifafanua kuhusu kuumia mguu wa kulia zaidi wakati gari lake limeonekana kupigwa risasi upande wa kulia Lissu anasema kwamba "Sio kweli kwamba ni mguu wa kulia tu ndio ulioathirika, maeneo mengine yaliyopigwa na kuumizwa vibaya ni mguu wa kushoto ulipigwa mara mbili ijapokuwa hakuna mfupa uliovunjika, mkono wa kushoto ulipigwa na kuvunjwa vibaya chini ya kiwiko".

Aidha, "kipande cha risasi kilitolewa kwenye kiwiko chenyewe, mkono wa kulia ulipigwa na kuvunjwa vibaya chini ya kiwiko. Risasi sita zilitolewa tumboni na nyingine imebaki karibu na uti wa mgongo".

Pamoja na hayo Lissu ameondoa utata ulikuwa ukihoji kwa nini Mwenyekiti wa Chama chake Freeman Mbowe alikuwa wa kwanza kufika hospitali  "Mbowe hakuwepo kwenye eneo la shambulizi lakini watu wengine walikuwepo.Mfanyakazi wangu wa nyumbani alikuwepo. Mke wa Waziri wa Madini Medard Kalemani ambaye tunaishi jengo moja alikuwepo. Kwenye jengo jirani anakoishi Naibu Spika Tulia, mfanyakazi wake wa nyumbani alikuwepo na ndiye aliyenikimbiza hospitalini".

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na Dereva wa Lissu (aliyebeba nguo Mkononi) mara baada ya kumfikisha  Mbunge Lissu hospitali ya General Dodoma siku aliyopigwa risasi.

"Baada ya kushambuliwa na wakati nakimbizwa hospitali, mimi ndiye niliyemwambia dereva wangu ampigie simu Mwenyekiti Mbowe na wabunge wengine kuwapa taarifa. Walifika hospitalini more or less muda huo huo niliofika mimi. Nilikuwa na fahamu muda wote mpaka nilipoingizwa theatre ndio nikapoteza fahamu" .

Mwenyekiti Mbowe anaishi upande wa pili wa Area D. Site 3 (ninakokaa mimi) na Sengia (anakoishi Mwenyekiti) zinatenganishwa na ukuta mmoja. Yote ni majengo ya TBA na njia yetu ya kwenda au kutoka bungeni na mjini ni moja.

Pamoja na hayo Lissu amefafanua sababu iliyompelekea yeye mida ile kuleke nnyumbani kwake ambapo mesema kwamba "Mimi na dereva wangu tulitoka bungeni saa saba mchana tukaelekea nyumbani kwangu Area D kula chakula cha mchana. Hatukukutana na mtu yeyote njiani na wala hatukusimama mahali popote mpaka tulipofika nyumbani. Tulianza safari ya kwenda Area D takribani saa saba mchana. Bunge lilikuwa limeahirishwa kwa ajili ya chakula cha mchana".


from MPEKUZI

Comments